Saturday, March 21, 2015

Anonymous

TANGA PAGUMU LAKINI...KOCHA WA YANGA AFUNGUKA!

Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm.
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amewatoa wasiwasi mashabiki wa timu yake na kusema kuwa ana nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa leo dhidi ya Mgambo, ingawa amekiri utakuwa mgumu kutokana na hali ya hewa na mazingira ya uwanja. 

Yanga ambayo imeweka kambi katika Hoteli ya Capital City, leo inatarajiwa kuwa mgeni wa Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani.Kocha huyo wa zamani wa Berekum Chelsea ya Ghana, alisema hana hofu na mchezo huo licha ya timu yake kutokuwa na rekodi nzuri uwanjani hapo, alisisitiza anachotaka kupata ni pointi tatu na kusisitiza kuwa mpira hauchezwi kwa historia. 

“Michezo ya mikaoni mara nyingi ni migumu kutokana na mzingira jinsi yalivyo, mfano huu uwanja una maji lakini tunatakiwa kupambana na kupata pointi tatu.“Mgambo ni timu nzuri, lakini mchezo wa soka hauchezwi kwa historia, timu iliyojiandaa vizuri na kutumia nafasi ndiyo itakayoshinda katika mchezo husika.” 

Msimu uliopita, timu hizo zilipokutana katika Uwanja wa Mkwakwani, Yanga ililala mabao 2-1 jambo linaloongeza ugumu wa mchezo huo.Mabao hayo yote mawili yalifungwa na waliopeleka kilio kwa Simba, Malimi Basungu na Fully Maganga ambaye alisababisha penalti iliyopelekea Msimbazi kulala bao la pili Jumatano iliyopita.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.