Watu wengi wanafikiria usupastaa ni raha tena ni rahisi, ohooo usupasta kazi ngumu. Unajua kabla hujawa supastaa, kweli kunakuwa na kazi ngumu ya kubembeleza wahusika wasikilize kazi yako kama wewe ni mwanamuziki au wakuone sura yako kama wewe ni muigizaji.
Na kweli unasota sana, ahadi unapewa nyingi na mara nyingine unakatishwa tamaa kabisa, kama ni mdada mtihani mgumu zaidi, hapo ndipo mafisadi wa sanaa watataka kuchukua nafasi wakutumie kidogo, kwa kweli kuna kazi ngumu.
Baada ya kuhaso, hatimaye unavuka unaanza kuwa maarufu, kazi zako zinaanza kusikika, unaanza kutajwa kwenye magazeti, hapo ndipo ishu ya kuanza kuitwa supastaa inapotakiwa.
Kabla ya kuwa supastaa unatakiwa uwe staa, lakini ndiyo hivyo tena, hii ni Bongo, ruksa kuwa supastaa bila kupitia ustaa. Halafu Kibongobongo wewe mwenyewe ndiyo unaanza kujiita supastaa, maana ukingojea Wabongo ndiyo wakuite utasubiri sana, sijui wakoje watakumezea hivihivi laivu.
Kwa hiyo ukiona umeanza kutajwa kwenye magazeti anza kujitambulisha kama supastaa. Ukipita sokoni, dukani mtaani kwenu anza kuwaeleza kuwa wewe ni supastaa. Yuko supastaa mmoja alikuwa anawatandika makonde madj kama akiingia mahala halafu hawapigi muziki wake na kumtaja. Pia anza kutembea na kundi la marafiki zako uwe unawanunulia bia moja moja wakatangaze kuwa sasa umekuwa supastaa.
Kama nilivyosema mwanzo, kuwa supastaa kazi ngumu sana. Kwanza lazima ubadili namna ya kuongea, usiwe unaongea kama watu wa kawaida hata kama umetoka Iringa au Mwanza lazima Kiswahili kibadilike, uwe unaongea unatupia neno la Kiingereza hapa na pale na kiwe kile Kiswahili kinachoonesha wewe umezaliwa Dar, lakini lazima ujiangalie kama muziki wako ni ara en bi Kiswahili chako lazima kiwe kama vile ulikuwa Ulaya miaka mingi sasa umerudi Tanzania kwa bahati mbaya, hivyo Kiingereza ndiyo unajua zaidi kuliko Kiswahili.
Itaendelea wiki ijayo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.