Hata hivyo, aina yoyote ya kuzuia mimba utakayoichagua ni lazima itumiwe kama ilivyoagizwa, ili kuleta matokeo ya hakika.Baadhi ya njia hizo kama vile kutumia kondom wakati wa ngono, pia kwa kiasi fulani humpa mtu kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya HIV na magonjwa mengine yanayoathiri afya ya uzazi.
Kwa vile mbinu za kuzuia uzazi ni za aina tofauti, ni muhimu basi uchague kwa makini ile inayokufaa. Utapata usaidizi wa kitaalam kama utashauriana na daktari wako, au pata usaidizi katika kituo cha kwenu cha upangaji uzazi, au kituo cha vijana.
Mbinu za kuzuia mimba (Contraception)
Hivi ni vifaa au dawa zinazotumiwa kwa minajili ya kuzuia mimba kutungwa wakati wa kufanya ngono.
Kuna zile zinazotumiwa kwa mda mfupi na nyengine kwa muda mrefu. Nyingine hufanya kazi papo hapo na nyingine huhitaji maandalizi ya muda.
Kondom au tembe maalum ndizo njia bora zinazojulikana zaidi za kuzuia mimba.
Pia kondom zina manufaa bora zaidi zinapotumiwa kwani mbali na kuzuia mimba zinapotumika kama inavyopaswa zinaweza pia kumkinga mtu asiambukizwe virusi vya HIV, na magonjwa mengine ya zinaa.
Vifaa vya kuzuia mimba.
Moja ya mbinu bora na rahisi za kuzuia mimba, ni kuweka kizuizi, kwa lengo kuwa mbegu ya mwanaume na ile mwanamke zisikutane. Kwa maana hiyo kifaa maalum kinaweza kuwekwa katika njia inayotumiwa na mbegu ya kiume ndiyo isilifikie yai la mwanamke.
Baadhi ya vifaa hivi (hasa kondom) pia vinaweza kukinga kuambukizwa virusi vya Ukimwi, na magonjwa mengine ya kuambukizana kupitia ngono.Kuna aina kadhaa za vifaa vya kuzuia mimba. Kondom za wanaume na zile za wanawake ndiyo vifaa vinavyofahamika zaidi, hata hivyo kuna pia vifaa vingine viitwavyo Diaphragm na Caps kwa kimombo ambavyo vinaweza kutumiwa na wanawake.

Note: Only a member of this blog may post a comment.