Martha Mboma,Dar es Salaam
BAADA ya kufanikiwa kunasa nyota watatu, uongozi wa Klabu ya Mbeya City, umefunguka kuwa hautafanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake na kwa sasa wanasaka nafasi moja pekee ya mchezaji ambaye anaweza kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani.
Mbeya City imefanikiwa kumnasa beki Haruna Shamte (JKT Ruvu), kiungo Joseph Mahundi (Coastal Union) na mshambuliaji Gideon Brown kutoka Ndanda FC huku wachezaji wake wawili, Deus Kaseke na Peter Mwalyanzi wakitua Yanga na Simba.
Akizungumza na Championi Jumatano, katibu wa timu hiyo, Emmanuel Kimbe, alisema kuwa kwa kiasi kikubwa kwa sasa nafasi zote zina wachezaji na wanasaka mchezaji ambaye anamudu nafasi zaidi ya moja.
Kimbe alisema kuwa, msimu ujao vijana watapewa nafasi katika kikosi chao, ndiyo maana hawasajili wachezaji wengi kutokana na kuwa na vijana wenye uwezo mkubwa.
“Tumeshawasajili wachezaji takriban watatu wa nafasi tofauti, kwa sasa tunaangalia nafasi kama moja na tunataka mchezaji mwenye uwezo mzuri na awe anamudu kucheza nafasi zaidi ya moja, yaani kiraka.“Lengo ni kuboresha kikosi lakini bado tuna wachezaji wengi wazuri vijana ambao tunaamini kabisa watapambana,”alisema Kimbe.

Note: Only a member of this blog may post a comment.