Na Haruni Sanchawa
MAMA mmoja
Aisha Ramadhani (26), mkazi wa Gongo la Mboto , Ilala jijini Dar es
Salaam amedai kuwa amekimbiwa na mume aliyemtaja kwa jina Athuman
Hussein baada ya kupooza kwa miaka miwili.
Akisimulia huku akitokwa machozi Aisha alidai: “Nimepooza kuanzia kiunoni hadi miguuni, mbaya zaidi miguu yangu kuna wakati inaniuma, inakuwa kama inapasuka hali ambayo imesababisha nishindwe kukaa achilia mbali kusimama.
“Nilikuwa na mume ambaye alikuwa akinipenda sana nami kumpenda na tukafanikiwa kumpata mtoto mmoja huyu (akamshika) Afsa, baada ya miezi kadhaa ya kuumwa, mume wangu akaingia mitini na kutuacha tukitaabika kwa njaa na ugonjwa.
“Baada ya mume kunikimbia mimi na mtoto wangu mwenye miaka minne tunasaidiwa na majirani na ….” Hakumaliza alichotaka kusema akawa anatokwa machozi huku akilia kwa kwikwi.Kwa yeyote aliyeguswa na habari hii anaweza kuwasilina na mama huyo kwa namba 0654 565423 au 0755 45 87 93.

Note: Only a member of this blog may post a comment.