Kesho ni June 13.. ni siku ya Kumbukumbu ambayo alifariki mmoja wa rappers wakali waliowahi kutokea TZ, Langa ambae
alifariki June 13 2013.. leo anasikika Mama mzazi wa msanii huyo ambaye
amesema aligundua kipaji cha mwanae tangu akiwa na umri wa mwaka mmoja
wakiwa Kigoma, alikuwa anapenda kucheza na kuimba pekeyake.
Afande Sele,
ni mmoja ya mastaa wa Bongo Fleva ambao waliwahi kupitia Jeshini, jamaa
alifukuzwa kwa kesi ya utovu wa nidhamu, unajua nini kilifanya
akafukuzwa?
Afande Sele
amesema alitimuliwa jeshini Chukwani Zanzibar baada ya kukutwa kwenye
maeneo wanayokaa askari wa kike, wakapelekwa kwenye makao makuu ya Jeshi
alafu baadae wakasimamishwa.
Msanii JI
aliwahi kuhit na wimbo wa kidato kimoja, leo kasikika akisimulia safari
yake mpaka kuingia kwenye muziki.. kumbe jamaa aliwahi kuwa fundi,
baadae akapitia mpaka kumiliki saluni.. mwisho wake akaingia kwenye
usanii wa muziki.
Sauti ya 255 iko hapa, ukibonyeza play hapa chini utazisikia stori zote....


Note: Only a member of this blog may post a comment.