Wednesday, June 3, 2015

Anonymous

TFF kuzindua jezi mpya za Stars leo

Said Ally, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), leo Jumatano linatarajia kuzindua jezi mpya za timu ya taifa ambazo zitakuwa zinatumiwa na timu zote za taifa katika mashindano mbalimbali zitakayoshiriki.

Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto, alisema jezi hizo ambazo zitazinduliwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, zitaanza kuvaliwa na kikosi cha Stars katika mchezo wake dhidi ya Misri.

“Kesho (leo) Jumatano tunatarajia kuzindua jezi mpya za timu ya taifa na kuachana na zile za zamani ambazo zitatumika na timu zote za taifa katika michezo yake mbalimbali,” alisema Kizuguto.

Mbali na uzinduzi huo ambao utafanyika katika Goden Jubilee Tower
pia kutakuwa na zoezi la ugawaji wa tuzo kwa baadhi ya makocha na wachezaji waliojitolea kwa namna moja ama nyingine kuifikisha Stars hapa ilipo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.