YELEUWIII! Katika hali ya kushangaza, sauti ya mpenzi
wa staa wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Naftal
Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ inayosikika akimtongoza Wema Sepetu imemfikia
Shilole na kusababisha azimie, Ijumaa Wikienda linakupa ‘ubuyu’ kamili.
BETHIDEI YA SHAMSA
Tukio hilo lililozua mtafaruku lilijiri wikiendi iliyopita kwenye
Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kulipokuwa na pati ya
bethidei ya mwigizaji Shamsa Ford.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho kilishuhudia tukio hilo
mwanzo-mwisho, saa chache baada ya kumalizika kwa shughuli ya kulishana
keki, waalikwa walishangaa kumuona Shilole akiishiwa nguvu na kudondoka
baada ya kusikiliza ujumbe wa sauti aliotumiwa kwenye simu.“We acha tu.
Ilikuwa balaa. Watu tulikuwa katika shamrashamra ya kulishana keki,
ghafla tukashangaa mwenzetu anaishiwa nguvu na kuanguka,” kilieleza
chanzo.
Chanzo hicho kilitiririka kuwa, ujumbe huo wa sauti ulisikika Nuh akimuimbisha Wema kwa maneno ya kimahaba.
“Nuh kajipambanua ileile. Kaimbisha mistari yote ya kimahaba, utafikiri alikaririshwa. Alijitahidi kushusha vesi tamu ili kumuingiza Wema kwenye himaya yake. Huwezi amini jamaa alizidisha mbwembwe kiasi cha kumwambia amkubalie kwani hamtaki Shilole tena.
WEMA AMTOSA
“Wema amesikika akikataa, akamwambia hawezi kuwa naye kwani ni shemeji yake na anamheshimu Shishi,” kilisema chanzo hicho.
SHILOLE AMFUATA NUH
Chanzo hicho kilieleza kuwa, baada ya kuusikiliza ujumbe huo, Shilole alimfuata Nuh kwa ajili ya kumsikilizisha lakini Nuh alijibu ‘mbovu’ ndipo Shilole alipomuomba ufunguo wa gari waliyokwenda nayo, akarudi alipokuwa amekaa awali.
APOTEZA ‘NETIWEKI’
“Aliporudi alipokuwa amekaa, Shilole alijikuta akiishiwa nguvu na kuzimia ambapo Aunt Ezekiel na kina JB (Jacob Stephen) walipofanya kazi ya ziada kumpepea, huku wengine wakihangaika kummwagia maji kunusuru afya yake.
“Walifanikiwa kumpandisha kwenye gari lake. Joto lilikuwa kubwa kufuatia hali hiyo maana kila mtu alishindwa kuelewa kilichotokea, hivyo Shilole, baada ya kuzinduka aliulizwa kilichomfanya azime ambapo aliwasikilizisha sauti hiyo kila mmoja akabaki ameduwaa,” kilieleza chanzo.
Ilielezwa kuwa, mwigizaji Aunt Ezekiel ndiye aliyeokoa jahazi kwa kulazimika kuendesha gari la Shilole na kumpeleka nyumbani huku Nuh akipandishwa kwenye gari la JB kumpeleka kwa ndugu zake.
“Inaniuma sana, Nuh kuendelea kunidhalilisha kiasi hicho wakati ni mwanaume ambaye ninamheshimu, tunakoelekea uzalendo utanishinda.
“Watu wananiona mimi mkorofi lakini kama ningekuwa napenda kuweka kila jambo wazi, hakuna mtu angeendelea kunifikiria vibaya.“Siwezi tena kuendelea kuumiza moyo wangu kila kukicha,” alisema Shilole ambaye anatumikia kifungo cha Basata kwa kutojishughulisha na sanaa kwa takriban mwaka mmoja kwa kosa la kucheza nusu utupu jukwaani.

Note: Only a member of this blog may post a comment.