Aliyekuwa mshambuliaji wa Azam, Gaudence Mwaikimba.
Na Martha Mboma
BAADA ya uongozi wa Azam FC kuwaacha wachezaji wake watatu kutokana na kumaliza mikataba yao, aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Gaudence Mwaikimba, amefunguka kuwa licha ya kuachwa ataendelea kucheza soka mahali pengine na hafikirii kustaafu kwa sasa.
Azam imeachana na wachezaji hao ambao wamemaliza mikataba akiwemo beki mahiri David Mwantika, Amri Kiemba aliyekuwa kwa mkopo akitokea Simba na Mwaikimba ambaye amedumu kwa muda mrefu ndani ya kikosi hicho.
Akizungumza na Championi Jumatano, mshambuliaji huyo alifunguka kuwa, ni kweli mkataba wake na klabu hiyo umemalizika na hakuna mazungumzo yaliyofanyika mpaka sasa.
Mwaikimba alisema kuwa yeye ni mchezaji huru, sasa anahitaji kuhakikisha anajipanga upya ili kukabiliana na ushindani kwa sehemu atakayokuwa msimu ujao.
“Ni kweli sipo Azam, lakini ninaamini nitapata timu ya kucheza na sifikirii kustaafu, kwa sasa uwezo bado ninao mzuri na baada ya kumaliza mkataba Azam hakuna mazungumzo yaliyofanyika kati yetu.
“Mpango wangu mimi bado ni kuendelea kupiga mzigo mahali popote kwa sababu ni mapema sana kusema niachane na soka kwa sasa, cha msingi ni mimi kujituma ili kuweza kukabiliana na ushindani uliopo kwenye ligi kwa sasa,” alisema Mwaikimba, mshambuliaji wa zamani wa Yanga.

Note: Only a member of this blog may post a comment.