Headlines zenye stori za Siasa zimeendelea kutawala.. Makongoro Nyerere
ni Mbunge anaewakilisha TZ kwenye Bunge la Afrika Mashariki, nae
alikuwa nyumbani kwao Butiama, hapa nimenukuu sehemu ya kile aichokisema
akiwa huko.
“Nina nia ya kutangaza nia lakini bado sijatangaza nia… kwanza tuzungumze kuhusu utaratibu wa CCM. Mkutano Mkuu utakaa tarehe 11 na 12 June ili kuisikia Rasimu ya Chama, kuithibitsha na kuipitisha… Sizuki na kuanza kuzungumza kabla ya ilani ya Uchaguzi.. Wanaoamua nani awe kiongozi sio huku kwenye Chama, ni Watanzania…“>>> Makongoro Nyerere.

Kwenye sentensi nyingine akasema hivi kuhusu wale wanaomzungumzia >>> “Huyo
mtoto wa Nyerere huyo ni mlevi kweli… mmewashtukia au vipi??.. Huyo
mtoto wa Nyerere huyo anapenda wanawake kweli.. sasa mlitaka nipende
wanaume? Nawapenda kweli na mimi nashukuru MUNGU mnanipenda kweli”>>> Makongoro Nyerere.
Makongoro Nyerere akamalizia hivi >>>“CCM
sio chama cha vibaka, ni chama cha walio wengi.. wakulima na
wafanyakazi.. turudishieni chama chetu, mnaenda nacho wapi? Kufanya
nacho nini? Alafu sisi mtuache wapi?”>>>
Utamsikiliza kwa urefu zaidi kila alichokisema kwenye sauti hii hapa chini mdau...
-via millardayo

Note: Only a member of this blog may post a comment.