Monday, June 15, 2015

Anonymous

Pale ambapo ishu ya kupima HIV inavunja ndoa…#HehaHeka June 15 (Audio)


Heka heka ya leo inatoka maeneo ya Ilala, Dar es salaam, inahusu mama wa bibi harusi kulazimisha maharusi wakapime kwanza kabla ya kuondoka kwenda kuishi pamoja. 

Kitendo cha mama wa bibi harusi na shangazi kulazimisha maharusi hao kwenda kupima kwa kulala mbele ya gari makusudi ili lisiondoke lilisababisha mvutano mkubwa miongoni mwa ndugu wa pande zote mbili ambao hawakuweza kufikia muafaka. 

Baada ya mvutano mkubwa awali bwana harusi alikubali kwenda hadi Hospitali ya Amana kupima akiongozana na bibi harusi pamoja na ndugu wa pande zote mbili  lakini walipofika gafla alikataa kupima kwa madai amedhalilishwa na kutaka arudishiwe fedha zake. 

Inasemekana kuna mmoja wa watu aliwadokeza ndugu wa bibi harusi kuwa bwana harusi ni mgonjwa ingawa bw ana harusi amekiri tayari alishatembea na mke wake muda mrefu.
Isikilize hekaheka yote hapa chini...

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.