Monday, June 15, 2015

Anonymous

HABARI PICHAZ: LOWASSA HAKAMATIKI!

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akiwapungia wananchi wa mji wa Mpanda, Mkoani Katavi waliojitokeza kumlaki, wakati alipofika kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi, alikofika jana Juni 14, 2015 kwa ajili ya kutafuta udhamini wa wanaCCM ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. alie mbele yake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah.
Mh. Edward Lowassa akipokea fomu zenye majina ya wanaCCM wa Mkoa wa Katavi  Juni 14, 2015, waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Bi. Elizabert Kashira. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 3440 mkoani Katavi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah akizungumza machache mara baada ya Mh. Lowassa (pili kulia) kukabidhiwa fomu za wadhamini wa CCM za kumuwezesha kutata ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Wengine pichani toka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mngeja, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Dkt. Aman Kaburou pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda, Beda Katani.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Mselem Said Abdallah akimkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa ili aweze kuwashukuru wanaCCM wa Mpanda kwa kumdhani ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkomo maelfu ya wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Mpanda, waliofurika kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoani Katavi  Juni 14, 2015.Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 3440 mkoani Katavi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.