Wednesday, June 3, 2015

Anonymous

MPENZI WA NICKI MINAJ, MEEK MILL AFUNGUKIA UHUSIANO WAKE NA MDADA HUYO!

Rapa, Meek Mill.
Los Angles, Marekani MPENZI wa rapa wa kike, Nicki Minaj, Meek Mill ameibuka na kusema uhusiano wao upo makini sana. Minaj kabla ya kuwa na Mill alikuwa akitoka na Safaree Samuels aliyedumu naye miaka 12 kabla ya kuachana mwaka jana.
Meek Mill akiwa na mpenzi wake Nicki Minaj.
Mill, 28, ambaye naye ni rapa tayari amemvalisha pete ya dhahabu ya uchumba yenye umbo la ‘moyo’ ‘hitmaker’ huyo wa Kibao cha Anaconda.
Wikiendi iliyopita alipaza sauti kupitia Jarida la The Fader, kuwa uhusiano wao ni wa ukweli lakini wanahitaji muda kuweza kujipanga kabla ya kuingia kwenye ndoa pamoja na kujifunza kutoka kwa wenzao.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.