Wednesday, June 3, 2015

Anonymous

MKE AUNGUZWA VIBAYA NA MUMEWE HUKO SONGEA KISA POMBE

MWANAMKE ajulikanae kwa jina la Mwasiti Juma ,mkazi wa Songea ameelezea matatizo yaliomkuta siku alipounguzwa na mumewe ajulikanae kwa jina la Muhammed Ally mkazi wa Songea vijijini kisa pombe. Mwanamke huyo ambae amekutwa na mkasa huo ambapo alipokutwa na mumewe nyakati za usiku wakati yeye akihudumia nguruwe kwa kutoa uchafu kwenye boma la nguruwe ndipo alipoingia mume wake na kumtaka aache kazi alizokuwa akizifanya na kumfuata jikoni ambapo Mwasiti alikuwa amembandikia mumewe maji ya kuoga ,mume huyo ndipo alipoanza kumshutumu mama huyo kwa kosa la kuchelewa kupika mpaka muda anao fika yeye kwanini hajamaliza kupika.
 
Pia baada ya kumsema Mwasiti ndipo baba huyo alipoamua kuchukuwa sufuria la maji lililo kuwa jikoni na kumwagia mama huyo ambae alikuwa amejifunga kitenge. Mashuhuda wa tukio hilo walipozungumza na mtandao huu walisema kuwa baba huyo amekuwa akimtukana Mwasiti kila anapokuwa akirudi nyumbani ambapo mara nyingi huwa anarudi akiwa amelewa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.