Monday, June 15, 2015

Anonymous

Mkataba wa MESSI wawavuruga wachezaji SIMBA SC!

Ramadhani Singano ‘Messi’.
Na Hans Mloli
BAADA ya kuibuka kwa sekeseke la mkanganyiko wa mkataba baina ya Ramadhani Singano ‘Messi’ na klabu yake ya Simba SC na kisha kupatiwa ufumbuzi na TFF, suala hilo sasa limetawala vichwa vya wachezaji wa timu hiyo na wamezungumza machache juu ya umakini unaohitajika kuanzia sasa katika masuala hayo.

Wachezaji waliozungumzia masuala hayo ni wale ambao wamebakiza mikataba yao mifupi klabuni hapo na wale ambao bado wapo kwenye mazungumzo na vigogo hao kwa ajili ya kuendelea kuitumikia timu hiyo msimu ujao.

Kiungo Awadh Juma alisema kwamba anaamini hakuna mwenye kosa kubwa katika hilo kati ya Messi na Simba lakini kilichotokea ni makosa ya kibinadamu ambayo yanaweza kutokea popote lakini kutokana na hilo amejifunza kuwa makini muda mwingine katika masuala hayo na si yeye tu bali akawataka wachezaji wote kuwa macho.

“Siwezi kusema kwamba kuna mtu amefanya makusudi katika hilo, naamini kuna makosa madogo tu ya kibinadamu yalijitokeza kati ya Messi na Simba lakini pia hili linatufunza kuwa macho na makini zaidi linapokuja suala muhimu kama hilo ili yasije kutokea haya yaliyotokea hivi karibuni na hii siyo kwangu tu bali iwe kwa wachezaji wote na klabu zote ili kuepuka haya mambo,” alisema Awadh.

Wachezaji wengine nao kwa nyakati tofauti ambao hawakutaka kutaja majina yao kutokana na sababu zao binafsi za kimaslahi nao walisisitiza suala la umakini katika kusaini mitakaba.

“Haya masuala si ya kuchukulia kawaida, ni masuala yanayogusa maisha, hivyo umakini unatakiwa wakati mwingine, inabidi kufuata taratibu zote ili uwe salama, vinginevyo unaweza kuja kutokea usumbufu mkubwa zaidi ya huu wa sasa uliomtokea Messi,” alisema nyota mmoja wa timu hiyo.

Messi na Simba wapo kwenye mgogoro wa kimkataba. Messi anasema alisaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo unaoisha Julai 2015 lakini klabu yake inadai ilimsainisha mkataba wa miaka mitatu hadi 2016.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.