Na Hans Mloli
KATIKA kuhakikisha kikosi chake kinafanya vizuri msimu ujao, Kocha wa Yanga, Mdachi, Hans van Der Pluijm, amekuja na mipango mizito ikiwemo ya kutenga siku 14 za kukaa na wachezaji wake nje ya Mji wa Dar es Salaam, siku chache kabla ya kuanza kwa ligi kwa ajili ya kuwapatia ‘silaha’ nzitonzito.
Pluijm ameliambia Championi Jumatatu kuwa anajua msimu ujao utakuwa mgumu na utachangamka zaidi, hivyo anapaswa kujipanga mapema na kuangalia anafanya nini ili kufanikiwa katika mitihani hiyo.
Kocha huyo pia ameongeza kwamba anafahamu kuwa wachezaji wake wengi waliofanikiwa kufanya vizuri msimu uliopita wakiwemo Mrundi, Amissi Tambwe, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, wazawa Simon Msuva, Salum Telela na wengine wengi, wanahitaji kucheza zaidi ya msimu uliopita, hivyo kufanikisha hilo atahitaji siku 14 kwa ajili ya kukaa nao na kuwapika vilivyo ili wawe bora zaidi ya awali.
Pluijm ambaye ameiongoza Yanga kutwaa ubingwa wa ligi katika msimu uliomalizika hivi karibuni, tayari ameanza programu ya mazoezi ya kuwanoa vijana wake tangu wiki iliyopita na leo watafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, Dar.
“Kazi ya msimu ujao siyo ndogo, tutahitaji kujipanga zaidi ili kuhakikisha hatufanyi vibaya. Wachezaji wangu walikuwa wazuri msimu uliopita na nitahitaji wawe zaidi ya hapo msimu ujao, kwa hiyo tutahitaji kitu kama mfumo wa kambi kwa muda wa siku 14 hivi kwa ajili ya kujiweka sawa zaidi.
“Tutakaa siku hizo ikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza ligi, hapo naamini tutakuwa tumejijenga vizuri kwa mapambano,” alisema Pluijm.

Note: Only a member of this blog may post a comment.