Hekaheka ya leo inatokea Tabata Dar es Salaam ambapo mama mmoja analalamika mtoto wake wa miaka saba anafanyiwa mambo ya ajabu na bibi yake, kuna wakati anamchukua usiku na kumpeleka mahali ambako wanakutana na kufanya mambo ya kishirikina.
Mtoto huyo amesema bibi yake huwa anakuja usiku na kumfunga kamba alafu anampeleka sehemu ambapo anakuta watu wengine wakiwa wamefungwa minyororo… wanapewa damu pamoja na nyama za watu na baadaye anamrudisha kabla hakujakucha.
Mama wa mtoto huyo anasema alihisi mtoto wake muda mrefu lakini hakuwa na wasiwasi kwani alikua anaogopa kumvunjia heshima mama yake mzazi… baada ya kuona tatizo linaendelea ameona ni bora watu wafahamu ili aweze kupata msaada.
Mama huyo amesema ameenda katika makanisa mbalimbali na anaamini ni Mungu pekee ndiye atakayemuokoa mwanae.
Timu ya #LeoTena imeahidi kumtafuta bibi wa mtoto huyo kesho ili tusikie kutoka upande wake pia.. Hekaheka ya leo iko kwenye hii sauti hapa, kama ulipitwa unaweza kuplay kumsikia mama na mtoto ambaye anafanyiwa vitendo hivyo.

-via millardayo

Note: Only a member of this blog may post a comment.