Tuesday, June 16, 2015

Anonymous

Linah Ajipanga Kutoa 'Tamko Kali' kwa Mahasimu na Kumuhusu WEMA SEPETU Kumchukulia Bwana Ake!

Star wa muziki Linah Sanga amesema kuwa bado ana dukuduku kubwa moyoni ambalo anajipanga hivi karibuni kulianika hadharani kwa njia ya tamko rasmi ambalo atalitoa kwa njia hiyo hiyo ya mtandao. 
Linah 
Baada ya kupitia kipindi kigumu cha misukosuko ya kusemwa na vilevile kutukanwa mitandaoni na kulalamika sana, star wa muziki Linah Sanga amesema kuwa bado ana dukuduku kubwa moyoni ambalo anajipanga hivi karibuni kulianika hadharani kwa njia ya tamko rasmi ambalo atalitoa kwa njia hiyo hiyo ya mtandao.
Kwa mujibu wa Linah kupitia mahojiano exlusive tuliyofanya naye, amesema kuwa tamko hilo kwa sehemu linahusiana na tuhuma za kulalamika kuibiwa bwana, kitu ambacho kinaendelea akiwa haoni sababu ya kuendelea kukaa kimya zaidi, na kuumia roho.

Linah amesema kuwa, kwa sasa anajipanga kuandaa waraka huu na kuanzia siku yoyote kutoka sasa, mambo yote kutoka moyoni mwa mrembo huyu anayetikisa chati za muziki ndani na nje ya Tanzania, yatakuwa hadharani.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.