Matumaini ya kupona kwa Bobbi Kristina
yamezidi kupotea huku familia yake ikiridhia mtoto huyo kurudishwa
katika nyumba ya mama yake wakiamini wakati wowote anaweza kupoteza
maisha.
Hata hivyo bibi wa Bobbi Kristina ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mwanamuziki wa Marekani marehemu Whitney Houston, ameonekana kuturidhia uamuzi huo.
Baba yake Bobbi Kristina amejitahidi kwa
kiasi kikubwa kupigania afya ya mtoto huyo tangu alazwe hospitali
mapema mwezi wa kwanza baada ya kuanguka bafuni lakini bado hali yake
inaonekana kutoridhisha.
Inasemakana familia yake imepanga mtoto huyo kurudishwa katika nyumba ya mama yake mzazi ambapo ataendelea kukaa huko.

Note: Only a member of this blog may post a comment.