KHA! Kuna madai
kwamba, Aunt Ezekiel alishaandikiwa talaka na ipo nyumbani kwa wazazi wa
aliyekuwa mumewe, Sunday Demonte, Temeke Mwisho jijini Dar.
“Hivi mnajua kwamba, Aunt alishaandikiwa talaka? Kama hamjui mjue sasa. Ipo Temeke kwa wakwe zake. Jamaa si yupo Uarabuni mahabusu, alisikia mkewe ana mimba ya Iyobo. Nadhani wanashindwa kumpa hiyo talaka kwa sababu walishakata mawasiliano naye tangu kitambo,” kilisema chanzo.
Aunt mwenyewe alipotafutwa juzi na kuulizwa kuhusu madai hayo, alisema:
“Sijui lolote kuhusiana na hilo, aliyesema kuwa nimeandikiwa talaka ipo ukweni kwangu ndiye angesema kila kitu yeye kwa vile anajua, mimi sijui.”

Note: Only a member of this blog may post a comment.