Charles Boniface Mkwasa wakati akikinoa kikosi cha Yanga.
Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Moroco.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemtangaza Charles Boniface Mkwasa kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Mkwasa anachukua mikoba iliyoachwa na Mart Nooij aliyetimuliwa kazi majuzi.
Kabla ya uteuzi huo, Mkwasa alikuwa Kocha Msaidizi ya Klabu ya Yanga.
Aidha TFF imemteua Kocha wa Zanzibar Heroes, Hemed Moroco kuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars.
Note: Only a member of this blog may post a comment.