Wednesday, June 17, 2015

Anonymous

FAHAMU NJIA SALAMA ZA KUZUIA MIMBA-3


Wiki iliyopita tulizungumzia njia ya kuzuia mimba kwa kutumia Caps ambayo ni ndogo kuliko Diaphragms, tunaendelea kuchambua njia hiyo kama ifuatavyo:

Caps inapowekwa mahali pake ndani ya uke, au kama ni Diaphramgms, huziba kilango cha mfuko wa uzazi hivyo basi mbegu ya mwanaume haitapata nafasi ya kupita.

Ukishaoneshwa na daktari jinsi ya kuipachika, baadaye unaweza kuipachika mwenyewe kabla ya kufanya mapenzi.
Kwa matokeo bora zaidi, Diaphragms na Caps hutumiwa pamoja na dawa iitwayo Spermicide ambayo huua mbegu za uzazi za mwanaume. Hapo Diaphragms au Caps humpa mwanamke kinga dhidi ya mimba kwa asilimia kati ya 92 na 98.

Hata hivyo, itachukua mazoezi ya muda ili kuvitumia itakikanavyo. Wakati mwingine pia hutumiwa na Gel yake maalum lakini bado havina hakikisho la asilimia moja kuzuia mimba.Faida yake nyingine ni kuwa, kwa kiasi fulani, vinaweza kukinga dhidi ya magonjwa ya zinaa na saratani ya lango la nyumba ya uzazi.

Ikiwa wewe hutumia vifaa kama Diaphragms au Caps, au hata kondom, ni vyema kujipangia mapema ndiyo usikose akiba, ndiyo haitakuwa karaha kuvitafuta pale unapovihitaji.

Mbinu nyingine za kuzuia mimba
Kuna chembechembe za kimaumbile, zinazojulikana vyema kama Homornes ambazo hutumiwa kutengeneza tembe au chanzo ya kuzuia mimba.Chembechembe hizi kwa jina maalum zinaitwa Progestogen.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.