Brighton Masalu
MAISHA
usiyapimie! Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amesema katika
harakati zake za maisha, aliwahi kugombea chakula na mbwa wakati akiwa
chuoni wilayani Bagamoyo, kitu ambacho kilimuumiza mno.
Makonda alitoa maneno hayo wakati akizungumza katika semina ya
kujikomboa kutoka katika umasikini inayofanyika kila Jumapili katika
Ukumbi wa Victoria Petrol Station, Makumbusho jijini Dar es Salaam
ambayo mhamasishaji mahiri nchini, Eric Shigongo hushiriki.
“Mama yangu alikopa Finca, hela hazikutosha ada, vitu vyake vyote vya ndani vikachukuliwa, chuoni nilikuwa nasubiri wenzangu wakishakula kantini, nawahi kula makombo kabla watu waliotoa oda ya chakula cha mbwa hawajaja. Wakati mwingine nililazimika kugombana na watu waliokuja kuwachukulia hao mbwa kama tukikutana.
“Siku moja Bi. Mkubwa alikuja shuleni na mzigo wa unga bila mboga,
hakuwa na chochote na wala mimi sikuwa na fedha. Nilifanya bidii kwenye
masomo hatimaye leo hii mimi ni mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Kwa simulizi zaidi ya Paul Makonda, usikose kufuatilia magazeti ya Global Publishers.

Note: Only a member of this blog may post a comment.