Monday, June 15, 2015

Anonymous

Baada ya Kupata Tuzo ya Kill Music, Yamoto Band Wameamua Kufuata Njia Alizopitia Diamond PLATNUMZ..Wameamua Kufanya Hili!

Kundi la muziki wa bongo flava nchini, Yamoto Band wanatarajia kukwea pipa kwenda Afrika Kusini kwa ajili yakufanya video ya wimbo wao ‘Cheza kwa Madoido’ na muongozaji mahili barani Afrika, Godfather.

Yamoto Band ambao usiku wa kuamkia jana walitwaa tuzo ya Kili katika kipengele cha ‘Kikundi bora cha muziki (Bongo Flava) wameamua kwenda Afrika Kusini kufanya video ikiwa ni hatua za awali za kuingia katika soko la kimataifa.

Aidha Yamoto Band wameachia video ya wimbo wao mpya unaoitwa ‘Nisambazie Raha’ unaofanya vizuri sana katika vituo vya radio iliyofanyika chini ya uongozaji wake Isangi Mental.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.