Wednesday, May 13, 2015

Anonymous

BREAKING NEWS: RAISI WA BURUNDI APINDULIWA NA JESHI!

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyepinduliwa.
Habari zilizotufikia hivi punde jeshi nchini Burundi limempindua Rais Pierre Nkuruzinza.
Meja Jenerali Niyombare ametoa taarifa kupitia moja ya kituo cha Radio cha Isanganiro kwamba serikali ya Nkurunziza imevunjwa
askari wazingira kituo cha utangazaji cha serikali nchini Burundi baada ya afisa wa jeshi kutangaza kuipindua serikali ya Nkurunziza.

NEWS UPDATES:
RIPOTI kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi.
Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpwito.
Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.
Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa rais huyo kugombea kwa  awamu ya tatu. 

Jenerali huyo alitimuliwa na Nkurunziza mwezi Februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.
Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.