Friday, April 17, 2015

Anonymous

SHEIKH AFUNGUKA MAZITO KUHUSU SABABU ZA WANAUME KUWA MASHOGA! MZAZI MTARAJIWA SOMA HII TAFADHALI...

Kiongozi wa kidini wa Iran, Dehnavi ni maarufu kwa kutoa mihadhara ya masuala ya familia na mahusiano
Kiongozi wa kidini mmoja nchini Iran anawafundisha wafuasi kwamba kufikiria mwanamke mwingine wakati wa kufanya ngono na mke wako kutawafanya wanao mashoga.
Ayatollah Hossein Dehnavi, mhubiri maarufu nchini Iran, alitoa hotuba kwenye hadhira kubwa ya wanaume na wanawake nchini mwake.

Alisema wanawake wasiojifunika watawafanya wanaume wao kuwa mashoga
Ni mafundisho ya utata kwa kipindi hiki kutolewa na Dehnavi, ambaye alionya kwamba kama wanawake hawatavaa hijab (kitambaa kinachoziba kichwa na kifua), wanaweza kusababisha wanaume wako kuwa mashoga.
Kwenye tukio la nyuma aliwahi kuhubiri kwamba wanawake wanalazimika kufanya mapenzi kwa wanaume wao muda wote na kusema kuwa wanawake ambao wanajitegemea zaidi kielimu au kifedha huwathiri uongozi wa wanaume.

Dehnavi anasema dunia itakuwa na amani kupitia mafundisho yake
“Moja ya majukumu ya wanawake kwa wanaume wao ni kujali mahitaji ya wanaume zao (ngono), kiongozi huyo alisema katika taarifa ya Clarion Project, taasisi inayopinga msimamo wa mawazo makali.
“Usiharibu ufahari wao na lazima muwe na hisia zaidi kwao.”

Anasema wanaume wanatakiwa kufanya mapenzi mara moja hadi mbili kwa wiki, wakifanya zaidi watashindwa kujizuia
Wakati wa hotuba nyingine, Ayatollah alieleza kwamba sio dhambi kwa mtu kufikiria kuhusu mwanamke wakati akifanya mapenzi na mwenzake, lakini ila akiwa mjamzito matokeo yake mtoto atakuwa shoga.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.