Wednesday, April 15, 2015

Anonymous

ALA KIPIGO KUTOKA KWA WATU WASIOFAHAMIKA NA KUFARIKI DUNIA

Saimeni Mgalula, Mbeya  
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Jaisoni Mwandenga (55) wa mkazi wa Kata ya Kaloleni wilayani Momba mkoani  hapa, hivi karibuni aliuawa kikatili kwa kupewa kipigo kikali kabla ya kupasuliwa kichwa na watu wasiofahamika. 

Akizungumza na gazeti hili, Afisa Mtendaji wa eneo hilo, Richard Mbwaga alisema Mwandenga aliuawa saa 8:30 za usiku, baada ya watu hao kuvunja mlango wa nyumba yake, kasha kumpiga na kitu kizigo kichwani kilitosababisha ubongo wake kumwagika, kabla ya kumtoboa mgongoni kwa kifaa aina ya sululu. 

Alisema chanzo cha mauaji hayo bado haijafahamika, lakini inahisiwa ni masuala ya kibiashara ambayo marehemu alikuwa akijihusisha nayo.Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutochukua sheria mkononi, badala yake wajenge mazoea ya kuwafikisha mbele ya vyombo vya dola kwa hatua za kisheria. 

Wakati akisema juhudi za kuwatafuta wauaji hao zikiendelea, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya serikali mjini Tunduma kwa uchunguzi zaidi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.