Tuesday, April 21, 2015

Anonymous

POMBE SIO CHAI JAMANI! Kilichomkuta Huyu, mmh ya MUNGU Mengi!

CDCOyijVAAAZHum
Don’t drink and drive..’ 
sawa hilo somo jamaa alilielewa sana tuu, akaenda zake kupata kinywaji ishu ikawa jinsi gani atarudi home??
Ilikuwa ni kama bahati yake tu kukutwa na gari za doria za Polisi ambao walimkuta mida ya saa kumi usiku, hajielewi.. amelewa sana alafu kalala katikati ya barabara.. hakuwa na jeraha lolote la kuumizwa wala hakugongwa, kilichomfanya aanguke katikati ya barabara ni ulevi. 

Jamaa aliwaambia Polisi  kwamba alitumia usiku wote kulewa, hata hapo alipo hajui kafikaje yani..!!
Ishu metokea New Zealand, ilibidi Polisi wambebe kumpeleka nyumbani kwake.. Polisi wamesema walevi wengi ni waathirika wa matukio ya kukabwa na kuibiwa usiku.
Umewahi kukutana na tukio gani mtu wangu na wewe ukasema ulevi noma? Nitafurahi kuona utakachoniandikia kwenye comment yako..

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.