Hii picha ya ajali nimeiona kwenye baadhi ya mitandao ya Nigeria, imenishtua nikaona niifatilie ajali imetokeaje.
Ajali imetokea Kano, Nigeria.. watu saba
wamefariki, Polisi wanafanya uchunguzi wa tukio hili.. ajali hiyo
imetokana na kuanguka kwa daraja la waenda kwa miguu lilil0kuwa
likiendelea kujengwa katika barabara.
“Mafundi
waliokuwa wanajenga waliwakataza watu wasipite na magari chini ya daraja
kwa sababu bado kazi ya ujenzi ilikuwa ikiendelea, huyo dereva wa taxi
alikiuka agizo hilo.. alikuwa anakatisha na gari ikiwa na abiria, daraja
likaanguka.. wamefariki watu saba..“– Magaji Majiya, msemaji wa Jeshi la Polisi.
Mara nyingi ujenzi ukiwa unaendelea
kwenye barabara kunakuwa na vibao vya maelekezo lakini watu wengi huwa
hawazingatii maelekezo, ndicho ambacho kimetokea kwenye hii ajali ya
Nigeria.
Picha nyingine za ajali hiyo hizi hapa..
Hii ajali abiria waliokuwemo kwenye taxi hiyo wala dereva hata hawakujua hiki kingetokea, #RIP kwa watu wetu waliofariki.

Note: Only a member of this blog may post a comment.