Bao
la dakika za usiku la Cesc Fabregas limeiwezesha Chelsea kuvuna pointi
tatu katika mechi ya ligi kuu soka nchini England ugenini dhidi ya
Queens Park Rangers (QPR).
Fabregas alifunga goli hilo pekee dakika ya 88' katika mechi iliyopigwa jioni ya leo uwanja wa Loftus Road.
Ushindi
huo umewafanya Chelsea wazidi kuota mbaya kileleni wakijikusanyia
pointi 73, pointi 7 dhidi ya Arsenal wenye pointi 66 katika nafasi ya
pili.
Hata hivyo Chelsea wana mchezo mmoja mkononi kwani mechi ya leo ni ya 31 wakati Arsenal wameshacheza mechi 32.


Note: Only a member of this blog may post a comment.