Tuesday, March 10, 2015

Anonymous

NOMA SANA: Mashabiki Wamshambulia Aunty Ezekiel kwa Nguo Anazovaa!

Baadhi ya mashabiki  wa Staa wa Bongo Movies, Aunty Ezekiel wameonyesha kuchukizwa na nguo anzaovaa Staa huyo ukizingatia kwasasa ni mjamzito. 

Kwa mara kadhaa Aunty  amekuwa akibandika picha mtandaoni huku akiwa amevaa nguo ambazo followers wake na mashabiki wamekuwa wakisema hazifai kuvaliwa na mwanamke mjamzito, kitu ambacho aunty mwenyewe na baadhi ya mashabiki wamekuwa mara zote wakisema ni sawa kitu ambacho mara zote husababisha mabshano na hadi kutoleana lugha chafu. 

Mbali na wengi kusema nguo anazovaa zinambana sana tumbo kitu ambacho sio kizuri wa ustawi wa kiumbe kilichopo tumboni,wapo wailosema mavazi hayo hayana heshma kwani kwa hali yake ya sasa inabidi ajistili  nasio kujiweka wazi wazi kama anavyofanya sasa. 

Mimi sio mjuzi sana wa maswala ya nguzo za wamama wajawazito ndiomana nimezileata hapa baadhi ya picha hizo ili wenye uelewa wa maswala haya watujuze  kuwa ni sawa au sio sawa...kwani kuna baadhi ya dada zetu wanapenda sana kuigaaaaaaa.
Mzee wa Ubuyu!
-via bongomovies

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.