Simba kwa hivi karibuni
imeonekana kufanya usajili kwa usiri zaidi, huwezi kusikia fununu za
kutangaza kumuhitaji fulani hadi uhamisho ukamilike, Simba imerejesha baadhi ya wachezaji wake wakongwe kikosini kama Musa Hassan Mgosi na Mwinyi Kazimoto hivyo baada ya klabu hiyo kutangaza kuhitaji golikipa mmoja aongeze nguvu kikosini, zilizuka tetesi za kutaka kurejeshwa kwa Juma Kaseja.
Juma Kaseja ni moja kati ya wachezaji waliowahi kuichezea Simba kwa mafanikio, kabla ya kuhamia Yanga, Kaseja ambaye ni mchezaji huru baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu zilikuwwepo fununu za baadhi ya viongozi wa Simba kumpeleka Oman akajifue ili aje ajiunge na Simba.
Lakini pia zilikuwepo fununu za mgawanyiko wa viongozi klabuni, wapo wanaoafiki Kaseja Kurudi na wapo ambao hawamtaki Kaseja, team ya millardayo.com ilibidi kumtafuta mkuu wa idara ya habari ya Simba Haji Manara kuweka sawa suala hilo.
“Kaseja
kurudi maana yake nini, Kaseja kurudi hakuna ulazima wa hilo maana yake
tukisema tumrudishe Kaseja itabidi tumrudishe na Mwameja tumrudishe Idd
Pazi aje kudaka tumrudishe kila mtu sasa kila zama zinagolikipa wake
mimi sidhani kama hata huo mvutano wa nini sasa huo mvutano Kaseja
alikuwa mchezaji wa Simba nadhani labda atakapo hitajika arudi atarudi”
>>>Manara
“lakini
kwa hivi sasa hatumzungumzii Juma Kaseja tunayo mipango mingine
itakapofika kama mfano benchi la ufundi likasema linamuhitaji Kaseja
tutalizungumzia right now hatuna mpango na Juma Kaseja”>>> Manara

Note: Only a member of this blog may post a comment.