Sunday, April 12, 2015

Anonymous

PICHAZ: MANCHESTER UNITED ILIVYOIFANYA KITU MBAYA MANCHESTER CITY OLD TRAFFORD

Baada ya kufungwa mechi nne zilizopita na Manchester Ciyty uwanja wa Old Trafford, Manchester United imejibu mapigo usiku huu ikiichapa City mabao 4-2 katika mechi ya ligi kuu.
Kipigo hiki kinazidi kuua matumaini ya Man City kutetea ubingwa wake ikizingatiwa jumatatu ya wiki hii walifungwa 2-1 na Crystal Palace.

Katika mechi ya leo, Man City walikuwa wa kwanza kuandika goli la kuongoza kupitia kwa Sergio Aguero katika dakika ya 8' kabla ya Ashley Young kusawazisha dakika ya 14'.
Marouane Fellaini aliifungia United bao la kuongoza dakika ya 27'  kabla ya Juan Mata kufunga la tatu dakika ya 67'.
Msumari wa nne umepigiliwa na Chriss Smalling dakika ya 73' kabla ya Aguero kuifungia Man City goli la pili dakika ya 89'.
-via mpenja

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.