Monday, April 20, 2015

Anonymous

AMUUA MPENZI WAKE KISA WIVU WA MAPENZI JIJINI TANGA

MKAZI mmoja wa Mapinduzi jijini Tanga, Alfan Hamad (46) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua mwanamke aitwae Mary Lucas (20) kwa sababu ya wivu wa mapenzi.

Akithibitisha mauaji hayo ofisini kwake jana Kamanda wa mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Zuberi Mwombeji alisema tukio hilo lilitokea April 18 majira ya saa 4.40 usiku.

Alisema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kimapenzi uliosababisha wapenzi hao ambao ni mahawara kutoelewana na hivyo kupelekea Hamad kufanya ukatili huo.



USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.