Kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab leo tena kimefanya shambulio
katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa katika mji wa Garowe huko Puntland
nchini Somalia.
Habari zinasema kuwa, shambulio hilo lilikuwa la kujilipua kwa mabomu limesababisha vifo vya watu wanaokaribia kumi wakiwemo raia nwa Kenya wawili.
Taarifa kutoka kutoka kwa Ofisa wa polisi ya mji wa Garowe, Mohamed Abdi amesema mlipuko huo umetokea mbele ya ofisi za Umoja wa Mataifa katika mji wa Garowe ambao ni makao makuu ya Puntland huko Somalia na kwamba umelenga basi lililokuwa limebeba wafanyakazi.
Wakazi wa mji huo wamesema shambulizi hilo limetekelezwa na watu waliokuwa na mabomu dhidi ya basi la Umoja wa Mataifa mkabala wa Ofisi za umoja huo.
Msemaji wa kundi la kigaidi la Al Shabab, Abulaziz Abu Mus'ab amekiri kuwa shambulizi hilo limefanywa na wanachama wake.
Shambulizi hilo la kujilipua kwa mabomu lililolenga Taasisi ya Umoja wa Mataifa limefanyika wakati Rais Hassan Sheikh Mohamoud wa Somalia na mwenzake wa eneo linalojitawala la Puntland, Abdiweli Mohamed Ali Gaas, wakitarajiwa kuhudhuria mkutano wa usalama katika eneo hilo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.