Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’.
Issa Mnally na Gladness Mallya/ Ijumaa Wikienda
Maskini!
Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza
Stone’ yu mgonjwa tena, safari hii ameibuka na kueleza maradhi ambayo
yanamsumbua akisema: ‘Ugonjwa huu utaniua.”
Awali Ijumaa Wikienda lilipokea taarifa juu ya kuumwa kwa Banza
ambapo ilielezwa kuwa, alilazimika kusafirishwa kutoka Mbeya hadi Dar
baada ya hali yake kiafya kuwa mbaya.
AJIKONGOJA
Hivi karibuni, gazeti hili lilimfuata nyumbani kwake Sinza ya Vatican jijini Dar na baadaye alijikongoja na kwenda kwenye Ukumbi wa Flamingo uliopo Magomeni ndipo akazungumzia kinachomtesa.
Banza ambaye siku hizi hupenda kujiita Roho ya Paka alisema kuwa kinachomsumbua ni maumivu ya kichwa hasa wakati wa jua kali.
KIZUNGUZUNGU
“Kichwa
kinaniuma sana hasa wakati wa jua kali, mishipa ya kichwa inaniuma sana
halafu nasikia kizunguzungu muda wote, sifahamu ni kwa nini,” alisema
mwanamuziki huyo akionekana kuwa na maumivu makali.
‘Banza Stone’ akiuguza ugonjwa.
Jamaa huyo alisema kuwa anaendelea na tiba akisaidiwa na mama yake, Hadija.“Kwa sasa nipo tu nyumbani, natazama afya yangu, ukweli nahitaji matibabu ya nguvu ili kunirejesha kwenye hali yangu ya kawaida,” alisema Banza.
MSAADA WA MADAKTARI
Hata hivyo, Banza alisema hataki kuomba msaada wa kuchangiwa fedha ili kupata matibabu ila anachoomba ni madaktari ambao wanafahamu tiba ya ugonjwa huo ili wamsaidie kimatibabu.
Si mara ya kwanza kwa Banza kuumwa kwani mara kadhaa alisharipotiwa kuwa hoi kwa magonjwa mbalimbali ikiwemo kifua.
KUTOKA KWA MHARIRI
Ijumaa Wikienda linamtakia Banza afya njema ili arejee jukwaani kuwapa burudani mashabiki wake na madaktari wanaoona wanaweza kumtibu, wajitokeze.
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!


Note: Only a member of this blog may post a comment.