Stori: Waandishi Wetu/Ijumaa Wikienda
SIKU chache baada ya
kuibuka utata mkubwa juu ya kichanga cha kike cha mwimba Injili maarufu
Bongo, Flora Mbasha huku mitandao ya kijamii ikieleza kwamba baba wa
mtoto huyo si aliyekuwa mume wa mwanamuziki huyo, Emmanuel Mbasha ‘Ima’,
familia ya mwanaume huyo inadaiwa kufanya kikao kizito jijini Dar ili
kupata ufumbuzi, Ijumaa Wikienda linakujuza.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na familia ya Mbasha,
familia hiyo ilikutana Jumamosi iliyopita nyumbani kwa Ima,
Tabata-Kimanga, Dar ili kulizungumza suala hilo na kuona kama wanaweza
kukubaliana kukilea kichanga hicho endapo ni damu yao.KIKAO CHAVUNJIKA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu kuwa, kikao hicho hakikufikia
muafaka kutokana ndugu hao kutofautiana kimisimamo kwani kila mmoja
alitoa mawazo yake.
MBASHA ANASEMAJE?Alipotafutwa Mbasha ambaye sasa anatamba na Wimbo wa Haribu Mipango ya Shetani ambao inadaiwa amekuwa akiutumia kama kijembe kwa Flora, alisema aachwe kwanza kwani suala hilo linamuumiza kichwa na ni la kifamilia zaidi.
“Naomba mniache kwanza, sipo vizuri kwa sasa,” alisema
CLIP YAONESHA MSIMAMO
Kwa mujibu wa ‘clip’ ya sauti yake (Mbasha) aliyoituma kwa Ijumaa
Wikienda mwishoni mwa wiki iliyopita, yeye ana mtoto mmoja tu, Elizabeth
Emanuel Mbasha ’Liz’ ambaye ana miaka kama kumi na moja.
Mbasha
alisema hajui nini kinaendelea na kwamba ameambiwa habari za Flora
kujifungua mtoto wa kike lakini yeye haoni kama habari hizo zinamhusu
sana!
MSIKIE“Mimi sijui niseme nini? Nimeambiwa kwamba Flora amejifungua. Kwa hiyo? Mbona yeye Flora hajaniambia, si anajua taarifa hizo hazinihusu? Amuogope Mungu, yeye angewaambia watu ukweli.”
Ijumaa Wikienda: “Kwa hiyo unataka kusema mtoto si wako?”
Mbasha: “Yeye anajua.”
NDUGU WA MBASHA
Ijumaa
Wikienda lilizungumza na ndugu mmoja wa Mbasha (jina lipo) ambaye
alizungumzia sakata la shemejiye kujifungua mtoto akiwa mbali na
nyumbani:
“Haiwezi kukubalika. Yeye kama alijua amegombana na Mbasha halafu ana mimba, anangejinyenyekeza akatulia mpaka azae.
KUMBUKUMBU ZA NYUMA“Haiwezi kukubalika. Yeye kama alijua amegombana na Mbasha halafu ana mimba, anangejinyenyekeza akatulia mpaka azae.
Mara baada ya ugomvi wao na kuondoka nyumbani miezi saba iliyopita, Flora aliwahi kunukuliwa na chombo kimoja cha habari akikiri kuwa na ujauzito na kusema: “Ndiyo nina mimba lakini siyo ya Gwajima.”
AZUNGUMZIA UNDUGU WAKE NA GWAJIMA
Hata hivyo, hivi karibuni, Flora alikazia tena maneno yake kwa kusema kuwa Mchungaji wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima ni anko (mjomba) wake kwa hiyo watu wajaribu kuliangalia hilo, hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mjomba‘ake.
KUHUSU MADAI KUWA MTOTO NI WA GWAJIMA
Mwanasheria: “Kwanza nataka kusema kwamba, chombo chochote cha habari ambacho kiliandika habari ya kumchafua Flora tutakishitaki. Iwe ni magazeti iwe ni mitandao ya kijamii. Wanaosema ni mtoto wa Gwajima ndiyo wanaomchafua Flora kwa sababu si kweli.”
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!



Note: Only a member of this blog may post a comment.