Mkali katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni jijini Dar, Aunt alifunguka
kwamba, mbali na kumzushia juu ya ujauzito huo, kuwa mara ya kwanza watu
asiowajua walieneza uvumi kuwa alikwenda nchini Marekani na mheshimiwa
huyo lakini aliwapuuza kwa kuwa alikwenda kwa kazi yake ya sanaa. “Kuna binadamu hawajali maumivu ya mtu mwingine, inawezekanaje mtu aanze kuropoka kitu kizito kama hicho tena mtu na familia yake, sasa mtu ambaye ndiye muhusika wa ujauzito huu anajisikiaje?
Aunt alitiririka kwamba, mbali na uvumi huo, pia alishangazwa na baadhi ya wabunge waliothubutu kuzungumza kuhusu yeye na waziri huyo tena bungeni kwenye kujadili vitu vya msingi badala yake wanazungumza mambo ambayo hayana kichwa wala miguu.
“Hivi inawezekana kweli kabisa wabunge ambao tunawaheshimu wanakwenda kuzungumza vitu vya ajabu bungeni?
Akiwa katika pozi.
“Wamenifanya nisiwe naangalia hata hilo bunge kabisa,” alisema Aunt. Staa huyo alimalizia kuwa mambo hayo yanampa wakati mgumu na kumuumiza kwa sababu madai yanayozungumzwa ni mazito huku yakiwa hayana chembe ya ukweli zaidi ya kuleta mfarakano kwenye familia ya waziri huyo ambaye pia ni mbunge.
Mbali na waziri huyo, pia Aunt alikanusha kuwa mimba kubwa aliyonayo si ya yule mcheza shoo wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo kama wengi wanavyodai.
Kuhusu hilo, gazeti hili lilizungumza na Mose Iyobo ambaye alisema kuwa anachojua ujauzito ni wa kwake lakini akashangazwa na uzushi usiokuwa na kichwa wala miguu.
Akiwa na shoga yake Wema Sepetu.
Baadhi ya mashabiki wa Aunt waliozungumza na gazeti hili walionesha
kubaki na alama ya ulizo kwamba kama Aunt anamruka Mose Iyobo na
amekasirishwa na tetesi za kuhusishwa na waziri huyo ambaye ni mume wa
mtu huku mumewe, Sunday Demonte akidaiwa kufungwa Dubai, je, mimba hiyo
ni ya nani?
INATISHA SANA: MAJAJI BONGO KUPIGWA RISASI, ===>>RIPOTI KAMILI HII HAPA!
JIUNGE
NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU
UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU
TENA!


Note: Only a member of this blog may post a comment.