Miezi takribani 10 tangu atimuliwe kutoka kwenye nafasi ya ukocha wa klabu ya Manchester United, David Moyes
ameelezea moja ya jambo lilokuwa linaisibu timu ya Manchester United
wakati wa utawala wake na kutishia mafanikio ya timu uwanjani.
Akihojiwa na jarida maarufu la soka la FourFourTwo, David Moyes ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Real Sociedad
ya Uhispania alisema tatizo kubwa lilokuwa linaisumbua timu lilikuwa ni
wachezaji wengi kuwa na uzito uliopitiliza (Ubonge), kitu
kilichopelekea aamue kuwapiga marufuku kabisa matumizi ya chips kwa
wachezaji wake.
“Ndio, ilibidi nipige marufuku chips“– Moyes.
“Ilikuwa
kwa sababu kulikuwa na wachezaji wengi ambao walikuwa na uzito
uliopitiliza na sikudhani kama chips zilikuwa nzuri kwenye diet yao,
hivyo nikapiga marufuku.”– Moyes
KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.
Note: Only a member of this blog may post a comment.