Sunday, February 8, 2015

Anonymous

Diamond Akanusha Kupewa Milioni 500 na Lowassa ili Ampigie Kampeni....Asema taarifa hizo zina lengo la Kumchafua Lowassa

Meneja wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, Babu Tale, amesema hawajawahi kupewa kiasi cha fedha Sh mil 500 na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ili wampigie kampeni za urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na Mpekuzi, Babu Tale alisema watakuwa wehu kukataa fedha nyingi kiasi hicho wakati wenyewe wanafanya muziki ili kupata fedha, lakini ukweli ni kwamba hawajapewa kitu chochote.

Alisema hata hivyo Diamond yupo tayari kumfanyia kampeni mgombea yeyote atakayetangazwa kuiwakilisha CCM. 

“Kama kweli tungekataa fedha hizo hata Mwenyezi Mungu angetulaani, ila naamini taarifa hizo zitakuwa zinasambazwa na wapinzani wa kisiasa wa kiongozi huyo kwa lengo la kumchafua, hajawahi kutupa ofa hiyo,”alisema Babu Tale.

Meneja huyo alitoa ufafanuzi huo baada ya hivi karibuni kuzagaa kwa taarifa ambazo si za kweli, kwamba walipokea kiasi hicho ili kumpigia kampeni Lowassa.
HATIMAYE WEMA SEPETU AFUNGUKA KUHUSU KUOLEWA! 
===>>SOMA ZAIDI HAPA!
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142.ASANTE NA KARIBU TENA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.