Thursday, December 22, 2016

Unknown

Jaji Mkuu Azishukia Mahakama za Tanzania!

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande amewakumbusha watumishi wa mahakama nchini kutoa haki kwa wakati ili wananchi waache kuzilalamikia.

Amesema tofauti na mahakama, sekta nyingine zikiwemo za elimu na afya zinatoa huduma kupitia taasisi za umma pia za binafsi akisisitiza kuwa hakuna mahakama za binafisi nchini zinazotoa huduma kwa wananchi, hivyo mahakama zinapaswa kutenda kazi zake kwa weledi kutoka haki bila ya upendeleo na kwa wakati.

“Hakuna mahakama za binafsi kama zilivyo sekta zingine hivyo mtu akikosa huduma bora katika shule za serikali anaitafuta huduma hiyo katika shule za binafsi vivyo hivyo katika sekta ya afya …. lakini kwa mahakama ni tofauti ndio sababu tunajitahidi kukarabati na kujenga majengo ya kisasa ya mahakama” amesema Jaji Chande. 

Jaji Mkuu Chande ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na watumishi wa mahakama kutoka mikoa ya Rukwa na Katavi waliokutana katika ukumbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga mjini Sumbawanga.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.