Thursday, December 22, 2016

Unknown

Jeshi la Polisi Laomba Msaada Kumtafuta Msaidizi wa Mbowe, Ben Saanane

Baada ya kukaa siku 33 bila kuzungumzia kutoweka kwa Ben Saanane ambaye ni msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, jana Jeshi la Polisi lilijitokeza na kuomba msaada kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia kupatikana kwake.

Aidha, hatua hiyo ya Jeshi la Polisi imetolewa wiki moja tangu Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu atoe tamko la kuitaka Serikali kueleza kama imemkamata au inamshikilia kada huyo aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba 18.

Mbali ya kutaka Serikali ieleze mahali alipo msaidizi huyo wa Mbowe, pia mwanasheria huyo alitaka ufuatiliwe ujumbe wa vitisho aliowahi kutumiwa kupitia simu yake ya mkononi na mtu asiyejulikana.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.