Thursday, December 22, 2016

Unknown

Askofu Akunwa na FagiaFagia ya Rais Magufuli!

Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini amempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kazi nzuri ya `fagiafagia’ na kusafisha uozo serikalini katika mwaka mmoja wa utawala wake na kwamba anaamini mwaka ujao utakuwa ni wa kuijenga nchi zaidi.

Ameyasema hayo katika mahojiano na moja chombo cha habari kuhusu maandalizi ya Ibada ya Sikukuu ya Krismasi ambayo mwaka huu kitaifa itafanyika mjini Bukoba, mkoa wa Kagera ikiwa ni njia ya kuwafariji wakazi wa mkoa huo, kutokana na maafa ya tetemeko yaliyowakumba Septemba 10 mwaka huu.
Katika kusafisha uozo, Askofu Kilaini amesema Rais Magufuli amesafisha wanafunzi hewa, watumishi hewa, mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma, mambo ambayo yalikwenda vizuri na kufanikiwa.

Akasema “Mambo yamekwenda vizuri katika mwaka huu wa kwanza tayari tumeona fagiafagia katika maeneo mbalimbali, sasa mwaka ujao tunatarajia utakuwa ni mwaka wa kujenga baada ya kuondokana na mambo yote mabaya”.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.