
Msanii wa filamu, Johari Chagula amefunguka kwa kusema kuwa
kwa sasa ana kiu yakumpata mume sahihi ambaye ataingia naye kwenye
maisha ya ndoa.
Mwigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja, amesema umri wake kwa sasa unamruhusu kuingia kwenye maisha ya ndoa
“Mimi ni mwanamke kamili, ni mtu mzima. Nimeshakuwa sasa, kwahiyo
kiukweli nina kiu ya mume,” Johari aliliambia gazeti la Mtanzania.
“Mungu akinipa mume bora, nitaolewa. Sitaki kuzungumzia sana mambo
yaliyopita, lakini muhimu kwa sasa ni mume,”
Mbali na hayo mwingizaji huyo amewataka kukaa mkao wa kula kwa ajili
ya filamu yake mpya ambayo amewashirikisha wasanii wachanga kutoka
mkoani Mwanza.
Note: Only a member of this blog may post a comment.