Video hii ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia leo alfajiri inawaonyesha walimu wakichangia kumpiga mwanafunzi mmoja ndani ya ofisi.
Walimu hawa wanaonekana si tu wanampiga mwanafunzi huyo kwa viboko, bali wengine wanampiga makofi ya uso, huku walimu wengine wakiwasihi wamuache mwanafunzi huyo kwani wanaweza kumuumiza.
Taarifa rasmi za tukio hili la kupigwa Mwanafunzi
Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo.
Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga vile.
Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl Esther Harembo wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video. Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao.
POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali.Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo.
=========
Mkuu wa shule ya Mbeya Day pamoja na baadhi ya walimu wamechukuliwa na jeshi la polis kwa mahojiano zaidi. Tukio hilo lilitokea 28. September.
Jumanne tarehe 24 mwalimu wa vitendo alitoa homework kwa kidato cha 3 A, kwa bahati mbaya mwanafunzi huyo hakuwepo, Jumatano wakati mwalimu anakusanya homework yule mwanafunzi alimwambia mwalimu kuwa jana yake hakuwepo alikuwa anaumwa.
Mwalimu alianza kumpiga makofi darasani lakini akaondoka naye hadi ofisini na kuwaambia walimu wenzake kwamba mwanafunzi huyo hakufanya homework ndiyo walimu wakamchangia kumpiga.
Hali ya mwanafunzi bado siyo nzuri kwani aliumia sana sehemu ya kichwa na machoni. Tayari Waziri Mwigulu Nchemba ameagiza walimu hao kuchukuliwa hatua za kisheria.
MWIGULU Nchemba, W MNN
Tazama Hapa Video:

Video kutoka katika mitandao ya kijamii ikiwaonyesha Walimu wakishirikiana kumuadhibu mwanafunzi. pic.twitter.com/VDNaZEoBY4— Swahili Times (@swahilitimes) October 6, 2016
Note: Only a member of this blog may post a comment.