Tuesday, April 5, 2016

Anonymous

Ustadhi Mbaroni Kisa Upotevu wa Mwanandoa!

IMG-20160331-WA0005
Ustadhi Swamadu Ramadhan Samata.
Stori: Makongoro Oging’, UWAZI
DAR ES SALAAM: Mwalimu Mkuu wa Chuo cha Madrasa ya Vingunguti, Wilaya ya Ilala jijini Dar, Swamadu Ramadhan Samata anashikiliwa na Jeshi la Polisi Buguruni kwa mahojiano kuhusu  upotevu wa mwanandoa Yassin Salum, 30, (pichani).
Taarifa zilizopatikana wiki iliyopita kwa baadhi ya polisi wa kituo hicho zilisema, Ustadhi Ramadhan anashikiliwa kwa uchunguzi wa madai kuwa, yeye ndiye aliyeonekana naye mara ya mwisho

Mdogo wa Yasin, Halsa aliliambia gazeti hili kuwa kaka yao ambaye ni mwalimu wa madrasa na Ustadhi mwalimu mkuu, alitoweka Machi 21, mwaka huu saa mbili usiku.
“Nakumbuka siku hiyo  akiwa na wenzake, walipofika Vingunguti walikaa nje ya madrasa ambapo Ustadhi anadaiwa kumtumia ujumbe kwamba afanye hima waonane usiku huo.
IMG_1961Salum akiwa na mkewe.
“Kaka alijiuliza kwa nini leo ustadhi ananitumia ujumbe mwingi, kuna nini? Ilipofika saa mbili aliwaaga wenzake na kwenda kumuona Ustadhi na tangu hapo hajaonekana, akipigiwa simu haipatikani.
“Tulimfuata chuoni tukakuta milango imefungwa, walioulizwa walisema alikuwa na Ustadhi. Ilipofika saa sita usiku ilibidi familia na wanafunzi wa chuoni kukutana.

“Wengine walikwenda hospitali mbalimbali na vituo vya polisi kikiwepo Kituo cha Polisi Stakishari na kufunguliwa jalada namba STK/RB/464/2016 na jalada Namba VING/PE/04/2016 la Vingunguti, kesho yake saa 12.30 asubuhi Ustadhi alifika chuoni, tulipomuuliza alisema atarudi, kila tukimuuliza anajibu hivyo.

“Hata hivyo, watu wana wasiwasi na Ustadhi, ikabidi itolewe taarifa polisi ambapo alikamatwa,” alisema mdogo wa Yasin.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, SACP Lucas Mkondya alipoulizwa na gazeti hili alikiri kukamatwa kwa Ustadhi Ramadhan.

“Tukio hilo lipo na polisi inaendelea na uchunguzi wakati huo ustadhi huyo tunamshikilia kwa mahojiano,” alisema.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.