Tuesday, April 5, 2016

Anonymous

Hawa Ndio Mastaa wa Bongo Ambao ni Watoto wa Kishua… Wasioshobokea Taito Hiyo

Makala Boniphace Ngumije
ASILIMIA kubwa ya vijana hutamani kuzaliwa na kukulia katika familia za ‘kishua’ maana angalau makali ya msoto yanapungua si kama ya vijana waliokulia uswazi. Kwa watu waliokulia kwenye familia hizo za kishua si jambo la kushangaza kuwaona wakijivunia maisha waliyozaliwa na kukulia.
Katika makala haya inawaelezea baadhi ya mastaa waliozaliwa katika familia za kishua lakini hawapendi kabisa kujulikana kuwa wanatokea familia hizo;
Nahreel
Emmanuel Mkono ‘Nahreel’
Nahreel
Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ ambaye ni mmoja wa wasanii wanaounda Kundi la Navy Kenzo ni mtoto wa wakili wa kujitegemea na Mbunge wa Musoma Vijijini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Nimrod Mkono.
Historia ya maisha ya wazazi wake inaonesha Nahreel amekulia katika mazingira ya kishua maana hata ‘hustle’ za gemu ni tofauti na vijana wengine hakuhangaika kiivyo, akiwa tu na umri wa miaka 14 tu baba yake alimnunulia piano na vifaa vingine vya muziki kwa ajili ya kujifunzia baada ya kuonesha kuwa ndoto zake zilikuwa huko.
Lakini katika hali ya kushangaza Nahreel hapendi kabisa kuhusishwa na  maisha ya wazazi wake wala nyumbani kwao alikokulia, hupenda watu kumchukulia yeye kama yeye, basi!

nisher-3-color-2Nisher
Nisher
Ni produza maarufu Bongo anayemiliki studio kubwa ya kutengeneza video iitwayo Nisher Records. Kama ilivyo kwa Nahreel, Nisher pia amekulia maisha ya mkate na siagi. Baba yake ni mtumishi wa Mungu maarufu Arusha, anaitwa Nabii Gear Davie anayeliongoza Kanisa la Huduma ya Ngurumo ya Upako yenye makao makuu yake Arusha.
Japo kwa kiasi kikubwa baba yake huyo amechangia Nisher kufikia mafanikio aliyonayo lakini hapendi kabisa kuhusishwa na kile anachokifanya baba yake wala maisha ya nyumbani kwao.
vanessa
Vanessa Mdee ‘Vee Money’
Vee Money
Vanessa Mdee ‘Vee Money’ alizaliwa Arusha lakini amekulia katika mataifa tofauti yakiwemo Marekani, Ufaransa na Kenya kutokana na wazazi wake kuhama kikazi mara kwa mara.
Baba yake Vee Money, Sammy Mdee (Sasa marehemu) alikuwa ni mwanahabari maarufu nchini, lakini kama ilivyo kwa wasanii waliotangulia hapo juu Vee Money anayetamba na ngoma iitwayo Niroge kwa sasa hapendi kabisa kuhusishwa na maisha ya kishua ya nyumbani kwao.
lucci
Luciano Tsere ‘Lucci’
Luciano Tsere ‘Lucci’ ambaye ni prudyuza wa muziki Bongo amekulia katika maisha ya kishua ambapo baba yake Dk. Patrick Tsere ni Balozi wa Tanzania nchini Malawi pia aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.