Kwa wafuatiliaji wa kisiasa mtakumbuka
jinsi mtandao ulioundwa na Kikwete na Lowasa ulivyotikisa siasa za
Tanzania toka miaka ya 1990's.
Hatimaye mtandao huu ulifanikiwa kuingia
madarakani mwaka 2005 na wakuu wa mtandao huo wakagawana vyeo kama ile
waingereza wanaita "spoils of war" , yaani matunda ya kugawana madaraka
yaliyotekwa.
Wakati zkikwete aliwasogeza ndugu jamaa
na marafiki zake madarakani, Lowasa kwa gia kubwa aliingiza kina Ole
wengi kwenye utawala wa mikoa na mashirika ya umma.
Lakini utawala wa tamaa tu na si kutumikia wananchi ulianza kuleta matokeo yasiyo tarajiwa.
Chama CCM kikakosa malengo baada ya vichwa kama Mangula kutimuliwa au kuondoka.
Mawaziri wakawa wengi na walikuwa wanabadilishwa kama circus.
Na kwa vile tamaa haikuishia kutawala tu
kwa wana mtandao, tofauti kubwa, na zinazotokana na tamaa ziliibuka
kati ya waasisi wa mtandao, yaani Kikwete na Lowassa.
Tofauti hizo na hatimaye ugomvi uliokuwa
ukiendeshwa kama gemu la chess, uliishia kuwamaliza wote wawili katika
kimsimamo wa kuuendeleza mtandao.
Watanzania lazima tumshukuru Mungu, kwamba ni tamaa ya madaraka na mali ndio imewamaliza wana mtandao.
Magufuli amefanya vema kwa kuanza kuibua
madudu ya kutisha ya uongozi ambao ulikuwa hautawali bali unajinufaisha
na utendaji wa serikali.
Ni vema utafiti wa kina ujafanywa na
wataalam wa sayansi ya jamii , na katika kipindi kifupi, ili madhara
mahsusi yatambuliwe, na hatua za kurekebisha zichukuliwe.
Kitu kinachoonekana dhahiri ni
kuubinafsisha ukusanyaji wa kodi, na kodi hizo kuingia mifukoni mwa watu
binafsi badala ya serikali ili kutumikia wananchi.
Source: JF


Note: Only a member of this blog may post a comment.