Sunday, April 3, 2016

Anonymous

KOLETHA wa Bongo Muvi Afanyiwa Kitu Mbaya Pub!

coletha
Stori: Gladness Mallya
MSANII mkongwe kwenye gemu la filamu Bongo, Koletha Raymond amejikuta katika wakati mgumu baada ya kulizwa zaidi ya shilingi laki tano na mfanyakazi wake.
Akipiga stori na paparazi wetu, Koletha alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Lion-Sinza, Dar kwenye pub yake ambapo mfanyakazi wake anayejulikana kwa jina la Anna aliyekuwa mhudumu aliyekusanya fedha za mauzo za siku tatu ambazo Koletha hakufika kazini na kuondoka nazo.

“Yaani nilihisi kuchanganyikiwa kwani siku tatu sikufika hapo pub, siku niliyofika nikakuta friji la vinywaji liko tupu na kwenye droo hakuna hela yoyote, nimekuwa nikimtafuta sana huyo msichana lakini hapatikani kwenye simu na anapokaa amehama, nimeamua kumwachia Mungu tu maana naona nikienda polisi nitakuwa napoteza muda wangu bure, nimeamua kuuza mwenyewe hapa pub kwangu maana hii siyo mara ya kwanza kuibiwa,” alisema Koletha.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.