Sunday, April 3, 2016

Anonymous

Jack Chuz, Mumewe Waiangushia Dua Ndoa Yao!

JACK3
Jack Pentezel na mumewe Gardner Dibibi.
Stori: Mayasa Mariwata
STAA wa filamu Bongo, Jack Pentezel na mumewe Gardner Dibibi wamefanya dua maalum ya kujivunia kutimiza miaka mitatu ya ndoa iliyopitia changamoto nyingi.
Akipiga stori na paparazi wetu, Gardner huku akisapotiwa na mkewe alisema ni jambo la kumshukuru Mungu kuifikia tarehe ambayo walifunga pingu za maisha (Machi 22) tangu waoane mwaka 2013, kwa kuwa ni mengi yanayoongelewa na changamoto zilikuwa nyingi.

“Sina budi kumshukuru Mungu, unajua ndoa za mastaa kudumu ni vigumu, mtu anaweza kuona ni safari fupi ya ndoa lakini tumekumbana na changamoto nyingi hadi kufika leo hii na kizuri kila siku ndiyo kwanza tunazidi kupendana japo wengi wamekuwa wakiomba ndoa yetu ivunjike, tumeamua kusoma dua Mungu azidi kuisimamia ndoa yetu,” alisema Gardner

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.